1 Kings 5:8-10

8Hiramu akatuma neno kwa Sulemani:

“Nimepokea ujumbe ulionipelekea na nitafanya yote unayohitaji katika kukupatia magogo ya mierezi na misunobari.

9

aWatu wangu watayakokota kutoka Lebanoni hadi kwenye bahari, nami nitayafunga mafungu mafungu yaelee juu ya maji hadi utakapoelekeza. Huko nitayatenganisha, nawe utaweza kuyachukua. Wewe utakidhi haja yangu kwa kunipatia chakula kwa ajili ya watu wa nyumbani mwangu.”

10Kwa njia hii Hiramu akampa Sulemani miti yote ya mierezi na magogo ya misunobari kama alivyohitaji,
Copyright information for SwhKC